Jump to content

User:Robert Ullmann/Mwananchi/30 December 2008

From Wiktionary, the free dictionary

User:Robert Ullmann/Mwananchi/header

aina
Hili linaweza kuwa tukio kubwa na la aina yake si tu kwa mwaka huu bali pia katika historia ya matukio ya uchomaji shule nchini. [1]
ajabu
Kuhusu taarifa kuwa bodi ya NDC haikuidhinisha fedha hizo kuidhamini Uhuru Capital Management, Kanali Simbakalia alisema itakuwa ni jambo la ajabu. [2]
ajili
MABILIONI ya fedha zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kusaidia wafanyabiashara wadogo yamekwama kutokana na urasimu mkubwa unaodaiwa kuigubika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeelezwa. [3]
akawa
Maisha ya Kazim yalibadilika ghafla, akawa ni mtoto wa kutoka familia ya kitajiri, sio maskini tena. [4]
akionyesha
N'nini?” “Pesa za watu,” Double P alijibu huku akionyesha kusawajika usoni. [5]
akiwa
Kamanda mganga alisema tukio hilo lilitokea Desema 27 Mwaka huu mara baada ya kumalizika kwa maziko ya marehemu Athumani, aliyefariki dunia akiwa amelazwa katika Hospitali ya Misheni Mvumi, wilayani Chamwino. [6]
alijibu
Kazim alijibu kuwa si lazima, yuko tayari kuishi hapo na kufanya kazi za ndani kama zipo kwani maisha yale ya mitaani hakuwa anayafurahia. [7]
ambao
Akisimulia tukio hilo, Andingenye alisema kutokana na mtoto huyo kuchoshwa na kusumbuliwa na ustaadh huyo aliamua kumshtaki kwa wazazi wake, ambao kwanza walimuonya, lakini mwalimu huyo wa dini alikana kufanya kitendo hicho. [8]
ambazo
Mahitaji ya mafuta katika nchi zenye viwanda, ambazo ndio wateja wakubwa wa bidhaa hiyo, yamekuwa yakishuka siku hadi siku kutokana na msukosuko huo, huku serikali za nchi hizo zikitaka mabadiliko katika teknolojia ya nishati inayotumika kuendeshea viwanda na magari. [9]
awe
Kwanza tabia ya kuwavamia wafanyabiashara ni imepitwa na wakati na kuwapiga faini ya laki tatu awe nazo au asiwe nazo ni mbaya sana kwa sababu kunawaumiza sana kiuchumi unamrudisha alipotoka kiuchumi ifike pahala mlipa kodi awe rafiki awe ni mdau mkuu wa uchumi katika nchi," alisema Rais wa Chama hicho. [10]
baa
Alikuwa ndani ya ukumbi wa baa, Zanzibar Hotel, mtaa wa Zanaki katikati ya jiji la Dar es Salaam. [11]
baadhi
POLISI mkoani Dodoma, wanawashikilia wakazi sita wa kijiji cha Chilembe wilayani Chamino,kwa tuhuma za kuhamasisha baadhi ya watu na kuchoma moto nyumba ya mwenzao anayehusishwa na kifo cha mtu aliyetambuliwa kuwa ni, Athumani Timetheo(18). [12]
bali
Tunakwenda Uganda si kwa ajili ya kusindikiza, bali kupambana na kuhakikisha tunafanya vizuri katika michuano hiyo kwani michuano hiyo ni kipimo tosha kwa timu yetu inayojiandaa kwa fainali za wachezaji wanaocheza ligi ya ndani itakayofanyika Ivory Coast mwezi Februari. [13]
basi
Meneja wa bendi hiyo, Hassan Rehani alisema jumla ya wanamuziki 25 na viongozi watandoka kwa basi maalum la kukodi tayari kwa onyesho hilo la funga mwaka lililoandaliwa na Hoteli ya Safari Park. [14]
bei
SERIKALI imeshangazwa na kitendo cha wafanyabiashara wa mafuta nchini cha kupandisha bei ya bidhaa hiyo wakati kuna akiba ya kutosha inayoweza kutumika katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa. [15]
bia
Lete bia nyingine,” kwa sauti ya kujiamini alimwagiza mhudumu aliyepita mbele yake. [16]
chache
Kwa baadhi ya shule matukio ya moto yaliweza kutokea zaidi ya mara moja tena ndani ya muda wa siku chache. [17]
elimu
Lakini jitihada hizo zinapaswa kwenda sambamba na mambo mengine muhimu ili kufanikisha lengo la kuwapatia vijana wengi zaidi elimu ya sekondari. [18]
eneo
Alisema kutokana na wizi huo wananchi wa eneo la Sota waliwabaini watu na kuwashambulia kwa kuwapiga mawe na marungu na kusababisha vifo vyao na pia kuwachoma moto. [19]
es
Jana, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuwa serikali haifahamu sababu za wafanyabiashara hao kupandisha bei ya mafuta. [20]
fedha
Maharamia hao wa Kisomali wamesababisha hofu kwenye Bahari ya Hindi kutokana na kuendeleza vitendo vya utekaji meli na kudai fedha nyingi ili waziachie. [21]
gani
Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Meja Jenerali Mstaafu, Said Kalembo aliipongeza timu hiyo kwa kutwaa ubingwa huo ambao utaurudisha katika ramani ya soka mkoa wa Morogoro na kuahidi kukaa na uongozi wa MRFA kuangalia jinsi gani ya kuwapongeza. [22]
gari
Mtapendekezaje kwamba sisi tupewe tuzo ya tako kwa kuthamini gari kuliko kompyuta. [23]
getini
Akapita getini na kuwapungia mkono wale walinzi, nao wakamjibu kwa kumpungia mikono. [24]
hao
Serikali imetoa kauli hiyo wiki moja baada ya wafanyabiashara hao kupandisha bei ya mafuta ghafla kwa madai kuwa shehena walizokuwa wakitegemea zinashindwa kuja kutokana na utekaji wa meli unaofanywa na maharamia wa Kisomali kwenye Bahari ya Hindi. [25]
hapa
Naibu waziri huyo pia alikanusha madai kwamba kupanda kwa bei ya mafuta kunasababishwa na meli zenye shehena ya mafuta kushindwa kufika nchini kwa kuhofia kutekwa na maharamia wa Kisomali na kusema kwamba madai hayo si kweli na hayana uhusiano na suala la kupanga kwa bei hapa nchini. [26]
hasa
Kwa ujumla ZNCCIA inasema kwamba bado Zanzibar inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kubadilika kwa fikra za watendaji wa serikali hasa wanaosimamia shughuoi za biashara pamoja na wakusanyaji wa kodi wanahitaji kufanya kazi aktika ulimwengu wa sasa. [27]
hata
Alisema sababu nyingi zinaweza kujitokeza katika kipindi hiki, lakini ukweli ni kwamba sababu zote hizo hazina ushahidi hata kidogo hivyo haziwezi kuwa sababu ya kupanda kwa bei ya mafuta katika vituo vya kuuza mafuta sehemu yoyote nchini. [28]
haya
Watu waje waone miondoko tofauti kama vile mganda katoka baharini , samaki ,wanaona haya wamefanywa vibaya ,taratibu usimkanyage na nyingine kibao. [29]
hii
Ninapenda kuchukua fursa hii kuwahakikishia wananchi kwamba serikali inafuatilia kwa karibu suala hili na itachukua hatua muafaka kila inapobidi ili kuhakikisha kuwa upatikanaji wa bidhaa za mafuta nchini unakuwa wa uhakika," alisema naibu waziri huyo. [30]
hivi
Awali wafanyabiashara hao walikuwa wakiuza mafuta hayo kati ya Sh1,300 na Sh1,400 lakini hivi katika kipindi cha kuelekea sikukuu ya Krismasi, yalipanda ghafla hadi kufikia bei ya kati ya Sh1,700 na Sh2,000 kwa petroli katika sehemu mbalimbali nchini. [31]
hizo
Mbinu zote hizo zinazotumiwa na CCM zina lengo la kuwaibia kura wapinzani huku wakijua mshindi anapotangazwa, wapinzani huenda mahakamani, lakini hurudi mikono mitupu kwa kuwa wao ndio serikali," alisema. [32]
humo
BAADA ya timu ya soka ya Mtibwa Sugar kutwaa Kombe la Tusker, Chama cha Soka mkoani humo (MRFA) kinatarajia kukaa na uongozi wa serikali ya mkoa ili kuangalia namna ya kuienzi timu hiyo kutokana na kuutangaza vyema mkoa wa Morogoro. [33]
huo
Kwa mujibu wa barua iliyotolewa na kusainiwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi jimboni hapo, Juliana Malange mgombea huyo wa Chadema hataruhusiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo ulioandaliwa kuziba pengo lililoachwa na Mbunge Richard Nyaulawa aliyefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu. [34]
huu
Desemba 28 mwaka huu majira ya saa 4.30 Asubuhi. [35]
huyu
Lakini kwa bahati mbaya huyu aliyependekeza tuzo ya tako kwa wanaoazimia kwenye mawarsha yeye mwenyewe amependekeza tu hatua zichukuliwe bila kuonyesha nani achukue hatua hii. [36]
ile
Naibu katibu huyo alifafanua kuwa mbinu nyingine ni ile ya kumwaga polisi vijijini ili kuwajengea hofu wananchi. [37]
jamaa
Nawashukuru marafiki zangu, jamaa zangu, majirani zangu, mume wangu, watoto wangu, ndugu zangu, maadui zangu, wazazi wangu, wafanyakazi wenzangu, mabosi wangu na zaidi wasomaji wangu kwa impact kubwa mliyofanya katika maisha yangu mwaka huu. [38]
jeusi
Alipofika katika eneo hilo hakuzubaa, alilifuata Land Cruiser jeusi lililoegeshwa karibu na geti, akafungua mlango na kuingia. [39]
juu
Alisema kuwa pamoja na CCM kutumia mbinu hizo chafu, bado CUF haitakata tama kudai haki na kuendelea kuwaelimisha wananchi juu ya kuacha tabia ya kuuza shahada zao. [40]
kabisa
Kwa hali hiyo, wasichana wengi wa Kiafrika walio shuleni wanalazimika kuchagua kati ya kuhimili aibu inayotokana na kuhangaika kujihifadhi na hedhi katika mazingira ya shule na hasa hali hiyo inapotokea wakati ambao hawakutegemea au kukataa kwenda shule kabisa kuepusha aibu. [41]
kadhaa
Rubeya hakupatikana licha ya kutafutwa mara kadhaa. [42]
kike
Uwepo wake katika eneo la Kakola lililo karibu na mgodi wa Bulyanhulu wenye pilika pilika nyingi za kimaisha na hata idadi kubwa ya watu kumeifanya shule hiyo kukumbwa na tatizo tete la utoro kwa wanafunzi linalosababishwa na wanafunzi kukacha shule ili kutafuta maisha kwa haraka na ujauzito kwa wanafunzi wa kike. [43]
kuona
Kamanda huyo alisema baada ya kuona hali hiyo, mganga, alishauri mgonjwa apelekwe hospitalini kwa matibabu zaidi. [44]
kwake
Alisema kufuatia minong’ono na makelele Yaled, alikimbia kuelekea nyumbani kwake, huku wananchi wakimrushia mawe, lengo likiwa ni kutaka kumuua. [45]
kwani
Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa Chama hicho Abdallah Abass amesema kwamba sasa hivi kilichobakia kwa wazanzibari ni maneno matupu yasioonesha dalili kwa kufufuka kwa uchumi kwani biashara ndio imefikia kikomo chake. [46]
la
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeenguliwa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Mbeya Vijijini baada ya mgombea wake, Sabwee Shitambala kuondolewa katika orodha ya wagombea kutokana na Tume ya Uchaguzi kukubali pingamizi dhidi yake lililowekwa na vyama viwili. [47]
lake
Hata hivyo, Bhai alisema kuwa wanamsaka mtendaji wa kijiji hicho ambaye hakumtaja jina lake kwa mahojiano zaidi. [48]
makali
MAMBO yanaweza kuwa yamebumburuka?” Aloyce alimuuliza Chaka huku akimtazama kwa macho makali. [49]
malengo
Tuliitumia kwa malengo maalum," alisema Kanali Simbakalia. [50]
mali
Baadaye tarehe 18 wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika na Stadi za Biashara (MUCCoBs) cha mjini Moshi nao walitangaza mgomo kwa kususa kuingia darasani na kufanya uharibifu wa mali pamoja na kuwashambuliwa kwa mawe na mchanga wahadhiri wa chuo. [51]
mama
Wanaharakati wa masuala ya elimu kwa wanawake nchini Zambia, Daphne Chimuka wa Jukwaa la Wanawake Wasomi Zambia (FAWEZA) na Barbara Chilangwa wa Kampeni ya Elimu kwa Wanawake (CAMFED) wanasema kipindi cha hedhi kinaweza kusababisha unyayapaa kwa watoto wa kike shuleni kwa kuwa katika tamaduni nyingi za Kiafrika mwanamke anachukuliwa kama mama wa familia. [52]
mazuri
Mahudhurio katika Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam ambao hutumiwa kila mwaka na BD kwa ajili ya michezo ya ligi hiyo yalikuwa mazuri. [53]
mbili
Baada ya kugombana kwa muda mrefu kuhusu uchimbaji wa nishati hiyo, serikali ilimtafuta mshauri mwelekezi kwa lengo la kutushauri namna ya kugawana raslimali hiyo na kwa sasa tayari amekwishawasilisha taarifa rasmi ya mapendekezo katika serikali zote mbili namna ya kugawana raslimali hiyo," alisema Khatib. [54]
meza
Waishiwa walicheka kwa nguvu lakini nusura mzee avunje meza alivyokasirika. [55]
mkoa
Akizungumza na Mwananchi kutoka Kigoma, mkurugenzi mkuu wa NDC wa wakati huo, Kanali Joseph Simbakalia, ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa huo, alisema taarifa hizo zinalenga kuchafuana na kwamba mambo yote yako bayana. [56]
mkononi
Angalia simu za mkononi. [57]
mkuu
Katibu mkuu wa Chadema, Dk. [58]
mpya
WASHAMBULIAJI wawili wa kimataifa wa Tanzania wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, Athumani Machuppa na Said Maulid watakuwa wageni rasmi katika uzinduzi wa albamu ya Dogo Mfaume iitwayo Kazi ya Dukanii utakaofanyika siku ya mkesha wa mwaka mpya, Desemba 31,2008 kwenye Ukumbi wa Luxury Pub Temeke Jijini Dar es Salaam. [59]
msalani
Mara Double P akanyanyuka na kuelekea msalani. [60]
mshangao
Vipi tena?” Salma alihoji huku akimtazama Double P kwa mshangao. [61]
mtu
Kisheria hatuwezi kupanga bei ya mafuta kwa sababu haizalishwi na mtu mmoja mfano. [62]
mwa
BAADA ya mizengwe ya hapa na pale iliyokuwa ikitolewa na Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD), hatimaye ligi hiyo maarufu mkoani humo ya Kili RBA imeanza mwishoni mwa wiki iliyopita ikizishirikisha timu 16, nne kati ya hizo zikiwa ni za wanawake. [63]
nalo
Nani aliyeondoka nalo wakati ni mimi ndiye mwenye nalo?” “Wewe!” walinzi wale walitamka kwa pamoja, mshangao ukizitawala nyuso zao. [64]
nao
Kutokana na muda mfupi tulio nao, timu yangu itaendelea na mazoezi mpaka kesho asubuhi kabla ya jioni kuanza safari. [65]
naye
Wale wezi wenzake walipoona hakuna mawasiliano yoyote kutoka kwa Kazim waliondoka, hawakuwa na habari naye tena. [66]
ndio
Madai hayo ndio pia yaliyoifanya CCM kumwekea pingamizi mgombea huyo. [67]
ndipo
Kamanda Andingenye alisema awali wazazi wa binti huyo mara baada ya mtoto wao kurudi likizo walimuomba ustaadh huyo amsaidie masuala ya kidini katika madrasa yake na ndipo ustaadh huyo alipoanza kushikwa na tamaa na kuanza kumlaghai ili afanye mapenzi na mwanafunzi huyo. [68]
ndiye
Inaamini Baba Joyce ndiye amehusika kumuua na kumfukia kwa siri ili kuhakikisha hakuna siri inayotoka nje kwamba yeye na mkewe wamehusika kufanya kitendo hicho cha aibu cha kumfukuza mtoto wao, eti kisa amepata uja uzito akiwa mwanafunzi. [69]
ndugu
Kufuatia maelekezo hayo ya mganga, ndugu wa Marehemu, walimchukua mgonjwa na kupeleka hospitali ambako alipatiwa huduma ikiwa ni pamoja na kutundukiwa chupa za damu za maji," alisema Mganga. [70]
nguvu
Ni kweli wahenga walisema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, lakini hatua hii ya NCCR-Mageuzi kujitoa kwa kuwa tu vyama vya upinzani havikuungana kusimamisha mgombea mmoja haikuwapa haki wanachama wake ya kuchagua au kugombea kiti hicho. [71]
nini
Waishiwa wateule, kwa nini hapa Tanzania, daima tuko upande wa watendewa kuliko watendaji? Hebu angalia maazimio mwisho wa warsha zote ambazo hatimaye mnene kwenye nguvu amesimamisha. [72]
nje
Alifafanua kwamba haiwezekani mafuta yakapanda hapa nchini peke yake wakati nje ya nchi yanakotolewa bei yake inazidi kushuka hivyo ni lazima Ewura itoe maelezo ya kutosha ya sababu za bei ya bidhaa hiyo kuzidi kwenda juu. [73]
njia
Idrissa Mshoro uamuzi huo ulifikiwa na baraza la chuo kama njia ya kuepusha hatari chuoni hapo kufuatia mfululizo wa migomo wa zaidi ya siku tatu uliofanywa na wanafunzi hao wakiushinikiza uongozi pamoja na mambo mengine kutoa matokeo ya wanafunzi 227 yanayoshikiliwa na chuo. [74]
nne
Alisema kuwa hii ni mara ya tano kwa Twanga Pepeta kutumbuiza Kenya ambapo mara ya kwanza ilikuwa wakati wa uzinduzi maalum wa vituo vya huduma ya tiba, mara ya pili ilikua kwa ajli ya kusheherekea Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, mara ya tatu ilikuwa ya kuadhimisha miaka mitatu ya Mandao wa Kimataifa unao jishughulisha na tafiti za Uchumi na mara ya nne kwa ajili ya uzinduzi wa mtandao wa simu wa Orange. [75]
simu
Naye alipotafutwa, Kaduguda aliieleza Mwananchi kuwa apigiwe simu baada ya dakika tano na alipotafutwa baadaye alishauri atafutwe Katibu Mwenezi, Said Rubeya. [76]
sio
Karibu mwaka wa 20 sasa kama sio zaidi mazungumzo ni hayo kwa hayo hivi leo ukifika bandarini dare s salaam ukitokea Zanzibar unapekuliwa na ukionekana na doti mbili tu za kanga au televisheni moja kwa ajili ya matumizi yao unalipishwa licha ya kuwa na vielelezo vyote," alisema Salim Turky ambaye ni Mwekezaji wa ndani. [77]
sita
JESHI la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia ustaadh wa madrasa, Dadi Ramadhani, 35, ambaye ni mkazi wa Mafiga mkoani hapa kwa tuhuma za kujaribu kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita wa Shule ya Msingi Kinondoni jijini Dar es Salaam. [78]
siyo
Kiswahili siyo lugha ngumu kwangu na kwako. [79]
suala
Lakini kama imeshindwa kuweka ukomo wa bei ya bidhaa hiyo muhimu, na badala yake imeiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) kukutana na wafanyabiashara wa mafuta kujadili suala hilo na kulitafutia ufumbuzi. [80]
swali
Pengine, swali ni kuwa kwanini BD wawang'ang'anie udhamini pekee wa TBL wakati yapo makampuni makubwa nchini ambayo yakiombwa yanaweza kudhamini mchezo huo. [81]
timu
Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa uongozi huo umeamua kumtupia virago Gabriel kwa madai kuwa si mchezaji wao kwani tayari alishauzwa katika timu ya Fanja iliyopo Oman. [82]
tuzo
HE jamani, mambo ya nishani ya viatu na tuzo la tako yameleta ubishi mkubwa sana. [83]
uja
Mama yake, Joyce alikuwa akiishi mitaani baada ya kufukuzwa kutoka kwa wazazi wake baada ya kupewa uja uzito akiwa mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Sandara iliyoko katika kisiwa cha Bahe. [84]
ule
KASHFA za ufisadi zimezidi kutanda baada ya serikali kuliagiza Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), kufanya uchunguzi wa matumizi ya zaidi ya Sh1.5 bilioni zilizotolewa kama mkopo kwa ajili ya upembuzi wa mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma na ule wa chuma wa Liganga. [85]
upande
Chama Cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar (ZNCCIA) kimesema Zanzibar imemalizwa kiuchumi na Tanzania Bara na sasa wafanyabiashara wakubwa wanahamishia shughuli zao upande wa pili wa Muungano. [86]
uso
Wakati anaingia tu, alikutana uso kwa uso na mwenye nyumba, alibaini kuwa hawakuwa watu wazuri kwa sababu ya staili iliyotumia kuingia ndani. [87]
vifaa
Haitoshi kuwa na vyumba vya madarasa kama vifaa vya kufundishia havipo au havitoshi, na hakuna walimu wa kutosha. [88]
vipi
Haisemi nani achukue hatua, wala kwa vipi. [89]
vya
Juzi Shitambala aliwekewa pingamizi na vyama vya CUF na CCM. Chadema ilimwekea pingamizi mgombea wa CCM kwa madai kuwa alisema uongo kuhusu mahali alipozaliwa. [90]
wako
Akizungumza na Mwananchi jana, kocha wa timu hiyo, Salum Mayanga alisema timu yake imejidhatiti kikamilifu na wachezaji wake wako katika hali nzuri. [91]
wala
Na wala hatuwezi kukubaliana na madai kwamba maharamia wa Kisomali ni chanzo cha kupanda bei mafuta. [92]
wale
Wachezaji wa timu hiyo ni Shaaban Nditi na Salum Swed na wale wa Zanzibar kama Soud Abdi na Abdalah Juma. [93]
wao
Alisema tayari wameshapata taarifa za pingamizi dhidi ya mgombea wao kwamba limetupiliwa mbali na lile la CUF na CCM kukubalika jambo ambalo alisema limezua utata ndani ya chama chake. [94]
wapi
Vipi shwari?” Badala ya kulijibu swali hilo, Aloyce naye aliuliza, “Umefika wapi?” “Niko Ubungo. [95]
watu
Wakati huohuo, CUF imesema kuwa kinazitambua mbinu zinazotumiwa na CCM katika kuhakikisha kinapata ushindi kwa kuvuruga daftari la wapiga kura na kuongeza idadi watu kwa miujiza, ikidai kuwa hiyo ndiyo silaha yao kubwa. [96]
wote
Hata hivyo, Mapunda alitetea kuwa wanahisa wote wawili wa hoteli hiyo ni Watanzania ambao ni wafanyabiashara wa muda mrefu hapa nchini. [97]
yeye
Hata hivyo, Gabriel ambaye inasemekana uongozi wa Simba umemuza kisirisiri lakini yeye amekataa kuuzwa huko kwa timu hiyo ambayo si chaguo lake. [98]
yuko
Alisema mchezaji pekee ambaye alidhani kuwa angechelewa kutokana na ruhusa katika timu yake ya Kuwait, Danny Mrwanda aliwasili juzi mchana na tayari yuko katika mazoezi na hakuna majeruhi. [99]
za
Kutokana na pingamizi lililowekwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) maombi yao yamezingatiwa na hivyo mgombea wa Chadema hataweza kuendelea na kampeni zozote za uchaguzi," inaeleza sehemu ya barua hiyo. [100]